Mfinyanzi Aingia Kasri Siti Binti Saad - Mohamed Hilal Nasra
- Malkia wa Taarab
Wapeni wa muziki wa Taarab wana deni kubwa kwa mwinbaji maarufu Siti Binti Saad mzaliwa wa Unguja, ambaye katika uhai wake na baadae, amejulikana kama Malkia wa Taarab. Malkia huyu aliuchukua muziki wa Taarab akaupa sura mpya, akaubeba na kuufikisha katika ngazi ya kimataifa. Licha ya kuwa waimbaji wengi wa Taarab wamekuja na kuondoka, hakuna ambaye amefikia kilele alichofika Siti Binti Saad. Hayati Shaaban Robert, ambaye nae alikuwa na kipaji cha pekee katika uwanja wa ushairi kwa lugha ya Kiswahili, alihusudu uimbaji na kushangilia maendeleo ya Siti kiasi cha kuandika kitabu juu yake. Kitabut hicho, 'Wasify wa Siti Binti Saad' ndicho kilichochora, kwa mara ya kwanza picha halisi ya Siti Binto Saad kama ilibyojulikana kwa machache waliomuenzi na waliotaka kuweka kumbukumbu yake kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Shaaban Robert wrote the first full biography Siti Bint Saad, the great Taarab singer from Zanzibar. This is the most recent biography.
EAN: 9789987449460